Tanzia : MWANASHERIA NA MWANASIASA MKONGWE DK. MASUMBUKO LAMWAI AFARIKI DUNIA


Mwanasiasa na mwanasheria mkongwe, Dkt. Masumbuko Lamwai amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Mei 5, 2020.

Dkt. Lamwai aliwahi kuwa mbunge wa Ubungo (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia CCM na kisha  kuwa mbunge wa kuteuliwa na Rais Benjamin Mkapa.

‪Kabla ya kifo chake, Dkt. Lamwai alikuwa Mhadhiri Mwandamizi (Senior Lecture) katika Chuo Kikuu cha Tumaini akifundisha masomo ya Sheria.

Dkt. Lamwai atakumbukwa kama Mwanasiasa machachari, mwanasheria nguli na mkufunzi mwandamizi (senior lecturer) wa Tumaini University.

Akiwa NCCR-Mageuzi, alikuwa na wanasiasa wengine wakongwe kama Mabere Marando, Marehemu Dk Sengondo Mvungi(RIP), Augustine Mrema, Makongoro Nyerere, Prince Bagenda, Ndimara Tegambwage, Stephen Wassira na wengine wengi.

Katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi wa 1995, NCCR-Mageuzi walitetemesha na kutingisha .Baadae alijivua uanachama wa NCCR na kuhamia CCM.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post