TAKUKURU MANYARA YAMREJESHEA NYUMBA MAMA MJANE ALIEPORWA NA AFISA MAENDELEO YA JAMII | MALUNDE 1 BLOG

Friday, May 22, 2020

TAKUKURU MANYARA YAMREJESHEA NYUMBA MAMA MJANE ALIEPORWA NA AFISA MAENDELEO YA JAMII

  Malunde       Friday, May 22, 2020
Na John Walter-Manyara

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Manyara (TAKUKURU) ,imefanikiwa kumrudishia Nyumba, mama mjane Antusa Duncan Kaaya,ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wilani Kiteto,akiitumia kujiingizia fedha kwa kuipangisha.

Imeelezwa kuwa Nyumba hiyo aliachiwa mjane huyo na mume wake aliefariki miaka minne iliopita, lakini muda wote amekuwa akiteseka huku mtumishi huyo wa serikali  Katika idara ya Maendeleo ya jamii akiendelea kunufaika na mali za hizo.

Mama huyo anasema kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuwalipia watoto ada kwa sababu nyumba hiyo ndio ilikuwa tegemeo la familia katika kupata kipato.

Mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Holle Makungu amesema kumekuwepo na vitendo vichafu vya watumishi kuwadhulumu haki zao wananchi wanyonge na wao kama mamlaka wamebaini kuwepo kwa vitendo hivyo na kwamba wataenda sambamba na watu wa aina hiyo.

Amesema  afisa huyo alipaswa kusaidia jamii kupata haki yake lakini badala yake amekuwa sehemu ya kuikandamiza jamii hivyo akiwa kama Kamanda wa TAKUKURU Manyara atahakikisha mtu huyo anachukuliwa hatua zaidi.

Akikabidhi mali hiyo kwa mjane huyo,mkuu wa wilaya ya Kiteto Tumaini Magesa amesikitishwa na kitendo hicho cha mtumishi huyo kudhulumu mali zake na kutaka hatua kali zichukuliwe dhidi yake.

Wananchi wameipongeza  Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Manyara (TAKUKURU) kwa hatua hiyo ya kumrudhishia haki yake mama huyo mjane.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post