RAIS MAGUFULI: ATAKAYEPOKEA VIFAA VYA KUPAMBANA NA CORONA NA VIKIPIMWA NA KUKUTWA NA VIRUSI HIVYO ASHITAKIWE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza kuwa mtu yeyote atakayepokea vifaa vya kupambana na Virusi vya Corona, vikishapimwa na Maabara Kuu ya Tanzania na kukutwa vina Virusi hivyo, basi ashitakiwe na apewe kesi ya jinai.

Rais Magufuli ameyabainisha hayo leo Mei 21, 2020, Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, mara baada ya kuwaapisha Mabalozi wa nchi mbalimbali , Mkurugenzi wa TAKUKURU na Katibu Tawala Mkoa na kuongeza kuwa vitu vya bure vina gharama.

"Kwa mtu yeyote atakayepewa vifaa vya kuzuia Corona, halafu mkavipima mkakuta vina Corona, huyo mtu apelekwe kwenye kesi ya jinai, Watendaji wajiepushe kupokea pokea, tutatengeneza Barakoa zetu na tutatumia vifaa ambavyo vitakuwa tested na Maabara zetu, Corona inaisha lakini tusije tukapandikiziwa

“Jana nilimuona Mtu mmoja wa NIMR anasema sijui anapokea vifaa gani? Kama ni vifaa vipitie Wizara ya Afya vikaguliwe kwanza, corona ni vita, katika hiyo misaada unaweza kuletewa barakoa zenye corona kwasababu tu wanaona trend yetu nzuri, vya bure vinaponza " amesema Rais Magufuli.

Awali wakati wa hotuba yake, Rais Magufuli amekiri kumpa usumbufu mkubwa sana Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, na kumpongeza kwa namna ambavyo alikuwa mstari wa mbele katika mapambano hayo licha ya kwamba hana taaluma ya Udaktari.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post