MSANII MKONGWE AY ALA SHAVU LA INFINIX NOTE 7 (BIGI MAKINI)


Msanii mkongwe katika industry ya muziki, "AY" anayetamba na kibao cha Danhela ala shavu la Ubalozi wa simu mpya ya Infinix NOTE 7.


Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, @infinixmobiletz waliweka viashiria vya ubalozi huo wiki iliyopita na siku ya Jumamosi, Mei 9 walithibitisha ubalozi huo kupitia LIVE Session ya Instagram iliyo onyesha wawakilishi wa Infinix wakifanya mazungumzo na AY kuhusiana na simu ya Infinix NOTE 7.
Infinix NOTE 7 imepewa jina la Bigi Makini, na ndiyo sababu kuu iliyopelekea Infinix kufanya kazi na AY, kwani wengi tunafahamu AY ni msanii mkongwe mwenye mafanikio makubwa mwenye kuheshimika kutokana na mchango wake katika game la muziki Tanzania.

Infinix NOTE 7 simu yenye umbo kubwa la inch 6.95 na speed ya ajabu ya G70 processor na kutokana na sifa hizi huenda Infinix NOTE 7 ndiyo simu yenye uwezo mkubwa na yenye kuvutia zaidi kwa mwaka huu wa 2020.
Ili kufahamu mengi zaidi kuhusiana na Infinix NOTE 7 na bidhaa nyengine za Infinix tafadhali tembelea kurasa zao za mitandao ya kijamii @infinixmobiletz


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527