DAVID SILINDE AWAJIBU CHADEMA BAADA YA KUFUTWA UANACHAMA...."MAAMUZI YAO NI YA KITOTO" | MALUNDE 1 BLOG

Monday, May 11, 2020

DAVID SILINDE AWAJIBU CHADEMA BAADA YA KUFUTWA UANACHAMA...."MAAMUZI YAO NI YA KITOTO"

  Malunde       Monday, May 11, 2020
Muda mfupi baada ya Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kuwafuta uanachama wabunge wake wanne, Anthony Komu (Moshi Vijijini), Joseph Selasini (Rombo), David Silinde (Momba) na Willfred Lwakatare (Bukoba Mjini) kutokana na kukiuka miongozo ya chama hicho, Silinde amezungumza  na kutoa tamko lake kuhusu uamuzi huo wa chama chake.

"Kwa mara ya kwanza pamoja ya kwamba nimesikia kwenye vyombo vya habari, kitu ambacho kimenishangaza ni uamuzi wa kitoto wa CHADEMA

"Huwezi kumfukuza mtu ambaye haujamuita, hujampa mashtaka yake maana mambo yote nilipaswa kuelezwa kwamba kosa lako ni hili, kuna utaratibu wa kumhukumu Mbunge, huo utaratibu haujafanywa.

"Naisubiri hiyo barua nitaiona na nitazungumza na vyombo vya habari kuhusu mustakabali wangu wa kisiasa.,” amesema Silinde na kuongeza;

“Nimekishughulikia hiki chama kwa miaka 10 nikiwa mbunge na mwanachama, mimi bado ni kijana mdogo sana, miaka 35, wameahidi kunishughulikia lakini mimi naahidi pale nilipoweka jasho langu nitahakikisha narudisha. "


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post