MANISPAA YA SHINYANGA YATOA MICHE YA MITI KWA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA


Afisa Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga (kulia) akitoa miti ya matunda bure kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambapo ni mwendelezo kwa manispaa ya Shinyanga kutoa miche ya miti ya kivuli na ya matunda kwa wananchi wanaoishi katika Manispaa ya Shinyanga katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Shinyanga Press Club - SPC), Shaban Alley ambaye ni mwandishi wa habari wa Star Tv akipokea miti ya miembe,miparachi na mipera kwa niaba ya Waandishi wa Habari (kushoto) ni Mwandishi wa Habari Gazeti la Majira Patrick Mabula. Manispaa ya Shinyanga inaendelea kutekeleza Kampeni ya Kuhifadhi Mazingira kwa kugawa miti ya matunda na kivuli bure.
Mwandishi wa Habari Gazeti la Majira Patrick Mabula akiwa amebeba miche ya miti ya matunda baada ya Afisa Mazingira wa Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga kukabidhi miche ya miti kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Mwandishi wa Habari Gazeti la Majira Patrick Mabulaakiwa amebeba miche ya miti ya matunda
Waandishi wa Habari wakichukua miche ya miti. Wa kwanza kushoto Mwandishi wa Habari Gazeti la Mwananchi, Stella Ibengwe ambaye pia ni Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga akiwa amebeba miche ya miti. Wa pili kushoto ni Katibu wa Mweka Hazina wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Ally Lityawi ambaye ni Mwandishi wa habari gazeti la Tanzania Daima akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Shinyanga Press Club - SPC), Shaban Alley ambaye ni mwandishi wa habari wa Star Tv na Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga Estomine Henry (wa kwanza kulia).

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527