KADA WA CHADEMA MDUDE NYAGALI "MDUDE CHADEMA" AKAMATWA KWA DAWA ZA KULEVYA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Mpaluka Nyagali Mdude (32) ambaye ni Kada wa CHADEMA Maarufu kwa jina la Mdude Chadema Mkazi wa Itezi Jijini Mbeya kwa tuhuma za kupatikana na Unga unaodhaniwa ni dawa za kulevya Aina ya Heroin.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatano May 13, 2020, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya  Ulirich O. Matei amesema mtuhumiwa alikamatwa  May.10.2020 Jioni katika msako ulioyofanyika maeneo ya Kadege Stendi, kata ya Forest, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya. Aidha, RPC Matei amesema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na kosa jingine la Uchochezi na upelelezi wa shauri hilo bado unaendelea.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527