ISMAEL ADEN RAGE AKAMATWA NA TAKUKURU KWA RUSHWA


Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismael Aden Rage amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za rushwa na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu kabla ya wakati.


Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo ilisema kuwa mnamo Mei 23, 2020, Rage ambaye ni Mkurugenzi wa Voice of Tabora alishikiliwa baada ya TAKUKURU kupata taarifa kutoka chanzo cha siri kikieleza kuwa Mbunge huyo wa zamani wa Tabora Mjini amedaiwa kuanza kampeni za uchaguzi kabla ya wakati.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya siri iliyotolewa ilieleza kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Simba akiwa katika maeneo kadhaa ndani ya manispaa ya Tabora kwa nyakati tofauti alikusanya wapiga kura ambao ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ngazi ya kata na matawi kwa lengo la kuwashawishi ili wampigie kura.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527