CHADEMA YAZUIA WABUNGE WAKE KWENDA BUNGENI.....YAWATAKA WAJIWEKE KARANTINI KWA SIKU 14


Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimetoa maelekezo kwa Wabunge wake wote, kutohudhuria tena vikao vya Bunge vinavyoendelea,na wajiweke Karantini kwa muda wa siku 14 na wasiende majimboni kwao kipindi hiki mpaka pale watakapothibitika hawana maambukizi ya Virusi vya Corona.


Taarifa iliyotolewa na  Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe leo Ijumaa May 1, 2020  imetoa maelekezo manne kwa wabunge wa chama hicho ambayo ni; Kutohudhuria vikao vya bunge au kamati za bunge,Kutofika eneo la Bunge Dodoma na Dar es Salaam, Wabunge wajiweke karantini kwa muda wa siku 14, wabunge wa chama hicho wasiende mikoani au majimboni bali wabaki Dodoma hadi itakapothibitika hawana maambukizi


Aidha, CHADEMA  pia wameshauri Bunge lisitishwe kwa siku 21 ili kuruhusu wabunge wote kwenda Karantini, Wabunge wote wapimwe pamoja na familia zao na Kamati za Bunge zifanye vikao kwa njia ya mtandao


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post