Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA OFISI YA UWT SHINYANGA NA FEDHA OFISI YA CCM KITANGILI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, May 7, 2020

Picha : MBUNGE AZZA HILAL ATOA MSAADA WA KOMPYUTA OFISI YA UWT SHINYANGA NA FEDHA OFISI YA CCM KITANGILI

  Malunde       Thursday, May 7, 2020

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamad (kushoto), akikabidhi Computer kwa Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shambuo Katambi, kwa ajili ya matumizi ya ofisi. 

 Na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, ametoa msaada wa seti moja ya Kompyuta kwa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Wilaya ya Shinyanga, pamoja na fedha taslimu shilingi 180,000/= kwa ajili ya kununua mifuko 10 ya saruji ili kusukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili.

Zoezi la kukabidhi Kompyuta na fedha hizo za kununua saruji limefanyika leo, Mei 7, 2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, na kushuhudiwa na wajumbe wa chama hicho akiwamo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ambaye ndiye aliomba msaada wa Kompyuta hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Kompyuta hiyo na fedha taslimu kwa ajili ya ununuzi wa saruji mifuko 10 ili kusukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili, Mhe. amesema yeye ni mbunge wa mkoa mzima, hivyo ana jukumu la kuhudumia wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga pamoja na chama chake kwa ujumla.

Amesema baada ya kuambiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kuwa Kompyuta ya UWT Wilaya ya Shinyanga ni Mbovu, akaguswa na kuamua kutoa msaada huo ili kazi za Chama zisiweze kulala sababu ya ubovu wa kifaa hicho na kutoa huduma kwa wananchi.

“Nimeamua kutoa msaada wa Computer kwenye ofisi hii ya UWT wilaya ya Shinyanga, na mimi UWT ndiyo wamenilea hadi nikapata ubunge, na baada ya kuambiwa na DC kuwa Computer yao ni mbovu ikabidi niitafute haraka, na leo hii naikabidhi rasmi ili iweze kufanya kazi za chama,” amesema Mhe. Azza.

“Computer hii ina thamani ya Shilingi Milioni 2, ambapo pia natimiza na ahadi yangu ya kutoa mifuko 10 ya saruji ili kusukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili, ambapo natoa pesa Taslimu Shilingi 180,000 ,” ameongeza.

Aidha amesema ameshachangia pia vifaa tiba katika kituo cha afya cha Kambarage mjini Shinyanga, ambapo ametoa vitanda vitatu kwa ajili ya wazazi pamoja na mashuka 30.

Naye Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Shambuo Katambi, amempongeza Mbunge huyo kwa kutoa msaada wa Computer ambao utasaidia kusaidia kazi za chama kusonga mbele, huku akimuomba aendelee na moyo huo huo wa kujitoa kusaidia jamii pamoja na chama.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, amempongeza mbunge huyo kwa kuitikia ombi lake na kutoa msaada huo wa Computer, pamoja na kuwabeba kidedea wanawake kwenye nafasi za uongozi kwa kuchapa kazi kwa bidii.

Pia Mboneko ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Shinyanga, kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na kuacha kufukiza watoto wadogo na kuwazuia wasizurure hovyo mitaani.TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamad (kushoto), akikabidhi Computer kwa Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Mjini Shambuo Katambi, kwa ajili ya matumizi ya ofisi. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog.

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Azza Hilal Hamad (kushoto), akikabidhi Computer kwa Mwenyekiti wa UWT wilaya yaShinyanga Mjini Shambuo Katambi, kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

Mbunge wa viti maalum mkoani Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (kushoto) akimkabidhi fedha taslimu Shilingi 180,000 katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Gregrory kwa ajili ya ununuzi wa mifuo 10 ya saruji ambayo itasukuma ujenzi wa ofisi ya CCM Kitangili.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akizungumza mara baada ya kukabidhi Computer na fedha Taslimu Shilingi 180,000 ahadi yake ya ununuaji wa mifuko 10 ya saruji.

Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Mjini  Hadija Magoma Hassani, akimshukuru mbunge Azza kwa msaada huo alioutoa.

Mwenyekiti wa umoja wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Shambuo Katambi akishukuru kwa msaada huo kutoka kwa Mbunge Azza.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Agnes Gregory akishukuru kwa msaada ambao ameutoa mbunge Azza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akimshukuru Mbunge Azza, kwa moyo wake wa kujitoa kusaidia jamii na chama katika nyanja mbalimbali zikiwamo huma za afya na elimu.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 blog.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post