WANAMGAMBO 44 WA BOKO HARAM WAFARIKI GEREZANI NCHINI CHAD


Wafungwa 44 wa kundi la wapiganaji wa msimamo mkali la Boko Haram waliokamatwa na jeshi la Chad mwanzoni mwa mwezi huu katika mkoa wa Lac wamekutwa  wamefariki dunia katika gereza usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii.


Wafungwa hao walikabidhiwa mahakama siku ya Jumatano baada ya kukamatwa katika operesheni ya jeshi la Chad dhidi ya shambulio baya lililogharimu maisha ya askari wa chad katika moja ya kambi za jeshi la nchi hiyo.

Wafungwa 48 kutoka kundi la Boko Haram walizuiliwa katika kituo kimoja nje ya mji mkuu wa Ndjamena na kukabidhiwa mahakama siku ya Jumatano. Lakini Alhamisi asubuhi, 44 kati yao walikutwa wamefariki dunia katika  chumba walimo kuwa wamezuiliwa, kulingana na mamlaka ya Chad.

Kulingana na uchunguzi wa daktari, wapiganaji hao walikunywa sumu. Ripoti yake ya vipimo, kulingana na taarifa ya mwendesha mashtaka wa Ndjamena, Youssouf Tom, inaonysha kwamba walitumia vidonge vyenye sumu iliyosababisha  washindwe kupumuaWote walikamatwa wakati wa operesheni iliyoitwa "Hasira ya Bohoma", iliyotekelezwa na jeshi la Chad kuanzia Machi 31 hadi Aprili 8. Karibu wanajeshi 52 wa Chadi na wapiganaji kadhaa wa Boko Haram waliuawa katika mapigano hayo


Credit:RFI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post