WAGONJWA WAWILI WA CORONA WAONGEZEKA ZANZIBAR, SASA WAMEFIKA 7 | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, April 5, 2020

WAGONJWA WAWILI WA CORONA WAONGEZEKA ZANZIBAR, SASA WAMEFIKA 7

  Malunde       Sunday, April 5, 2020

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza uwepo wa wagonjwa wawili wapya wenye maambukizi ya virusi vya corona visiwani humo na sasa jumla wamefikia saba.

Taarifa ya Waziri Afya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed imeeleza kuwa wagonjwa hao ni raia wa Tanzania ambao kwa nyakati tofauti waliingia visiwani Zanzibar kutokea mkoani Tanga.

Mohamed amesema watu hao waliingia kupitia bandari ya Mkokotoni mmoja ni mwanaume mwalimu wa shule wa mkoani Tanga aliingia Machi 18 na mwingine ni mfanyakazi wa hoteli (27) alienda Tanga Februari na kurudi Machi 13.

“Wagonjwa wote wanaendelea na matibabu katika kituo cha matibabu ya corona cha Kidimni na hali zao zinaendelea vizuri” imeeleza taarifa ya Mohamed


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post