WENYE VIRUSI VYA CORONA NCHINI KENYA WAFIKA 142


Kenya imethibitisha kuwa na wagonjwa wapya 16 wa corona, baada ya kuwafanyia vipimo watu 530.

Hadi sasa Kenya imefikisha idadi ya watu 142 wenye maambukizi ya Corona.

Wizara ya afya nchini Kenya imetaarifu kuwa katika visa vipya 16, raia wa Kenya ni 15 na mmoja anatokea Nigeria.

Raia 11 kati ya hao wana historia ya kusafiri nje ya nchi ilihali 5 ni raia wa eneo.

Watu 12 ni kutoka mji mkuu wa Kenya Nairobi, wengine watatu wanaishi Mombasa 3 na mmoja kutoka Kilifi.

Waliokutwa na maambukizi mapya ni wennye umri kati ya miaka 22 na 66, wanaume ni tisa na wanawake saba.

Kati ya waliothibitishwa, tisa walikuwa kwenye karantini tayari.

Wizara ya afya pia imeweka wazi kwamba inatengeneza barakoa ambazo zitasambazwa kwa wananchi hivi karibuni.

Wizara ya afya imeeleza kuwa watu watakaokufa kutokana na virusi vya Corona watazikwa ndani ya saa 24 huku watu wa karibu wa familia wasiozidi 15 wakiruhusiwa kuhudhuria mazishi hayo yatakayoandaliwa na Serikali.

-BBC


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post