WAGONJWA WA CORONA NCHINI KENYA WAFIKA 234....NI BAADA YA WENGINE 9 KUONGEZEKA LEO

Idadi ya wagonjwa wa virusi vya coronavirus nchini Kenya  sasa imefikia 234 baada ya watu 9 zaidi kuthibitishwa kuambukizwa ugonjwa huo.


Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye amelihutubia taifa hilo leo Alhamisi  April 16 akiwa Ikulu ya Nchi hiyo.

Kenyatta amesema kwamba serikali ilipima sampuli zingine 704 kwa muda wa saa 24 zilizopita na ndipo hao  watu  tisa wakathibitishwa kuugua. 


Uhuru pia amesema idadi ya watu 53 wamepona kabisa na kuruhusiwa kwenda nyumbani tangu janga hili lilipotangazwa kuingia nchini humo

Aidha ametangaza kuwa watu 11 wamepoteza maisha yao, wengine 1,000 wakisalia karantini na wengine 156 wakitengwa katika sehemu mbalimbali nchini humo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post