VH.SHAH WAUZA SUKARI KWA BEI "CHEE" KANDA YA ZIWA
Na Charles  Mseti - Mwanza

WAKALA na msambazaji mkubwa wa sukari katika mikoa ya kanda ya ziwa VH. Shah, ameendelea kuuza sukari katika mikoa hiyo kwa bei elekezi inayotakiwa na Serikali.

Hivi karibuni, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, aliwaonya baadhi ya mawakala "wapigaji" wa sukari nchini kuacha kupandisha bei kwa madai ya kwamba bidhaa hiyo imeadimika nchini huku akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa atakaebainika.

Msimamo huo wa SHAH ni njia moja wapo ya utekelezaji wa agizo la Serikali la kuwataka wasambazaji (mawakala) wa sukari nchini kuuza sukari kwa mjibu wa taratibu.

Akizungumza jana, amesema sukari yote iliyopo katika maghahara yake, inatauzwa kwa watu wote bila kubagua mtu au mfanyabiashara yeyote yule.

Pia amesema, bei ya sukari inayouzwa (na wao) ni bei ya chini ya bei elekezi iliyoelekezwa na Serikali huku akisisitiza kuwa hakuna sababu ya wao kupandisha bei.

"Sisi tunauza sukari mpaka chini ya bei elekezi, lakini unaweza kushangaa leo tumeuza sukari ya kilo 50 kwa Tsh.130000 lakini kesho ukakuta tumeuza chini au zaidi ya hapo.

"V.H.Shah hatujawahi kupandisha bei na tunafanya kazi kwa mjibu wa sheria hatuwezi kufanya kosa la kupandisha bei ya sukari, tunafahamu tukipandisha bei ni kosa na tunaweza kufutiwa hata leseni na tunafanya kazi hii kwa kusasaidia wananchi wetu " amesema Shah.


Amesema kazi ya kusambaza sukari kanda ya ziwa wanaifanya kwa kufuata sheria na kanuni za biashara za nchi pamoja na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK. John Magufuli, anaepambana kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa kati.

"Rais wetu Magufuli anafanya kazi ya kuhakikisha nchi hii inakuwa na uchumi kupitia viwanda, sasa sisi tunafanya kazi hii ili kusaidiana nae, lakini unakuta kuna watu wanaongea mambo ya kwamba sisi tumepandisha bei kitu ambacho sio kweli," amesema.

Pia amewaondoa wasi wasi wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahakikisha kuwa sukari ipo ya kutosha na hakuna bei iliyopandishwa ya uuzwaji wa sukari.

Mkoa wa Mwanza, sukari ya KG 50 inauzwa kwa Tsh. 130000 huku mfuko wa KG 25 ukicheza kwa Tsh. 60000, ambapo bei hiyo ni kwa jumla. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post