BODI YA PAMBA YASHAURIWA KUDHIBITI UUZAJI HOLELA WA PEMBEJEO KISHAPU

SALVATORY NTANDU

Baada ya Kuwepo kwa Malalamiko ya Wakulima wa zao pa Pamba Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga ya kuwatuhumu Viongozi wa vya Msingi (AMCOS) kuuza pembejeo zilizotolewa na serikali kwa mkopo kwa wakulima hatimaye Bodi ya Pamba Tanzania imeanzisha  msako  mkali katika maduka ya pembejeo ili kubaini undani wa suala hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kuanza msako huo Aprili 18 mwaka huu, Mkaguzi bodi ya pamba, Thomas Daudi alisema kuwa watafanya ukaguzi kwenye maduka ya pembejeo ya watu binafsi pamoja na minada na magulio yote wilayani humo ambayo pembejeo hizo huuzwa kwa wakulima.

Daudi alifafanua kuwa ofisi yao imepokea malalamiko kutoka kwa wakulima wa pamba kuwa wapo baadhi ya  viongozi wa AMCOS wanauza kuuza pembejeo za kuulia kinyume na maelekezo ya serikali kwani pembejeo hizo zinatolewa kwa mkopo kwa wakulima kupitia vyama vyao vya msingi.

“Niwatake viongozi AMCOS kuacha tabia hiyo pamoja kwani watakapobainika katika msako huo watachukuliwa hatua kali za kisheri na pia wafanyabiashara walionunua  pembejeo hizo kunyume na utaratibu wanapaswa kuzisalimisha kwa Bodi ya pamba mara moja”,alisema Daudi.

Rajabu Masunga ni mkulima wa Zao la Pamba wilayani Kishapu aliyeshuhudia msako huo aliipongeza Bodi ya Pamba kwa kuwabana wauzaji wa pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali ambapo wengi wao walikuwa wakipanga pembejeo hizo chini kwenye minada na kuwauzia wakulima kwa bei ya juu.

Alisema kuwa pembejeo hizo ambazo ni sumu za kuulia wadudu katika zao la pamba katika minada mbalimbali huku kishapu zimekuwa zikiuzwa kiholela tena kwa kuanikwa juani na wakulima wengi wamekuwa wakizikosa katika AMCOS zao na kulekezwa kununua katika minada kinyume na maalekezo ya serikali.

“Tunashangaa siku ya mnada ambayo ni alhamisi ya kila wiki katika manada huu  mkubwa wa mifugo ambao pia wafanyabiashara huleta biashara mbalimbali hususani dawa za kuulia wadudu kwenye mazao ya mifugo ambayo wengi wetu hatujui kama ni yanavigezo vinavyotakiwa ama ni yale ya ruzuku yaliyotolewa na serikali,” alisema masunga.

Sambamba na hilo Masunga aliishauri bodi ya pamba kila siku ya Alhamisi ambayo ni siku ya mnada kufanya ukaguzi wa pembejeo zinazouzwa  ili kuhakiki kiwango cha ubora wa dawa zinazouzwa kwa wakulima ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kumkomboa mkulima.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post