22 WAPONA CORONA 1,126 WAPIMWA KWA SIKU


Nchi ya Uganda mpaka sasa imeripoti visa 55 vya waathirika wa Virusi vya Corona, na 22 kati yao tayari wamekwishapona huku 33 waliobaki wakiendelea na matibabu.

Aidha kwa mujibu ya taarifa ya vipimo vya sampuli vya watu 1,126, vilivyochukuliwa siku ya jana ya Aprili 18, 2020, vimeleta majibu ya kwamba wote hawana maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo kati yao madereva wa malori ni 837 na waliosalia ni wale watu waliokuwa wakifuatiliwa kwa ukaribu.

Aidha mpaka sasa nchi ya Uganda haijaripoti kifo chochote cha mgonjwa wa COVID-19, tangu nchi hiyo ianze kupata maambukizi hayo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527