
Askari wa kituo cha polisi Kia, Sajenti Juma Ango amekutwa akiwa ametupwa mtaroni mita chache kutoka kituo cha polisi Hai Mjini mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amesema watu waliokuwa wakifyeka majani kandokando ya barabara ndiyo waliokutana na mwili huo.
Sabaya amesema mwili huo umekutwa ukiwa na na jeraha kubwa kisongoni na kwamba alikuwa amepigwa na kitu chenye ncha kali.
"Taarifa zinasemekana alikuwa na askari wenzake jana hadi saa nane usiku maeneo ya Msami,"amesema Sabaya.
Social Plugin