MUME AMUUA MKEWE KWA KUMTWANGA RISASI..AJARIBU KUJIUA


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Elibariki Geofrey mkazi wa Chekereni wilayani Arumeru, kwa tuhuma za mauaji ya mke wake Ester Elibariki, baada ya kumpiga risasi mbili kifuani na shingoni, kisha na yeye kujijeruhi nayo shingoni, na sasa anatibiwa kwenye Hospitali ya Mount Meru.

Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Koka Moita, ambapo amesema kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Aprili 23, 2020, majira ya saa 6:25 usiku, ambapo taarifa za awali zinabainisha kuwa mauaji hayo ya kikatili yamesababishwa na wivu wa mapenzi.

"Tukio hilo limetokea eneo la Chekereni, wilayani Arumeru, Mama aitwaye Ester Elibariki aliuawa kwa kupigwa risasi mbili na mume wake Elibariki Geofrey, mwili wa marehemu huyo upo katika Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi, uchunguzi unaendelea ili kubaini nini chanzo halisi cha tukio hilo, japo taarifa za awali zinaonesha kuwa ni wivu wa mapenzi" ameeleza Kamanda Moita.

Aidha Kamanda Moita akielezea maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo, amesema kuwa katika Kijiji cha Morala Kata ya Songoro, kumetokea kifo cha mzee mmoja ambaye aliangukiwa na ukuta wa nyumba yake na kufariki pale pale.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527