MFANYAKAZI WA MAHAKAMA MBARONI KWA TUHUMA YA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 10 MAHAKAMANI SHINYANGA



Na Salvatory Ntandu - Shinyanga
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Joseph Masanja (58) mlinzi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Wilaya ya Shinyanga kwa tuhuma ya kumbaka Mwanafunzi mwenye umri wa Miaka 10 wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.

Tukio hilo lilitokea tarehe 21 Machi mwaka huu ambapo inaelezwa kuwa mtuhumiwa alimdanganya binti huyo aliyekuwa na mwanzake mwenye umri wa miaka saba kwenda katika eneo lake la kazi kwa madai ya kuwapatia fedha za kununua ndala.

 Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi leo Alhamis Aprili 2,2020 Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema mtuhumiwa alikamatwa baada ya binti hiyo kutoka katika eneo la kazi majira ya saa kumi na moja jioni.

“Ilikuwa saa nane mchana siku ya Jumamosi,mabinti hao walifika mahakamani, Joseph aliagiza binti wa miaka saba kubakia getini na kisha yeye kuingia ndani binti huyu na kumbaka katika moja ya chumba cha ofisi katika eneo la Mahakama”,alisema Magiligimba.

Magiligimba alifafanua  kuwa baada ya  Joseph kutekeleza tukio hilo alimwamuru binti huyo kuondoka eneo la tukio kwa kupitia geti jingine ambapo mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi aliyefahamika kwa jina moja la Leticia alipomkamata binti huyo na alimhoji kuwa ametokea wapi ndipo alipokiri alikuwa akifanya mapenzi na mlinzi huyo.

“Pia kuna Afisa wa polisi alimwona binti wa miaka saba aliyekaa getini muda mrefu,alipomhoji kwanini amekaa kwa muda mrefu katika eneo hilo alijibiwa kuwa anamsubiri mwenzake tangu majira ya saa 8 mchana alipoingia ndani na Mlinzi huyo hajatoka”,aliongeza Magiligimba.

"Askari huyo alimchukua binti huyo na kuingia naye ndani ya eneo la mahakama na kukutana na mwalimu aliyemkamata binti wa miaka 10 wakati akipitishwa geti la pili na Joseph,ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa wazazi wa mabinti hao",alieleza Magiligimba.

Aidha alisema kuwa baada ya mabinti hao kufikishwa polisi wazazi wao walifika na kupewa kibali cha kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo na vipimo vilibaini kuwa binti wa miaka 10 ameingiliwa (amebakwa)

Hata hivyo Magiligimba alisema,baada ya Joseph kutekeleza tukio ,alikimbia kusikojulikana hadi alipokuja kukamatwa na jeshi la polisi na Alipohojiwa alikiri kumbaka mwanafunzi huyo,na upepelezi wa tukio utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527