WATU 284 WATHIBITIKA KUWA NA UGONJWA CORONA TANZANIA.... KATI YAO, 10 WAMEFARIKI,11 WAMEPONA 256 WANAENDELEA VIZURI


Wagonjwa wa corona Tanzania wafikia 284, Waziri Mkuu wa nchi ya Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza.


Akihutubia katika tukio la ibada ya kitaifa jijini Dar es Salaam leo Jumatano, Majaliwa amesema kufikia Jumanne Aprili 21 wagonjwa waliothibitika nchini humo ni 284 ambapo kati yao 256 wanaendelea vizuri, saba kwenye uangalizi maalumu, 11 wamepona na 10 wamefariki dunia
.

Kufikia Jumatatu Tanzania ilikuwa imethibitisha wagonjwa 254, na hivyo wagonjwa 30 zaidi wameongezeka nchini humo.

Majaliwa pia amesema jumla ya watu 2815 waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1733 hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284).

Kutokana na taarifa hiyo wa Waziri Mkuu, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa mchanganuo wa Ongezeko hilo la Wagonjwa kimkoa.

Ameandika;Jumla ya watu waliopata maambukizi ya  #COVID19 nchini sasa ni 284 kutoka 254 tuliowatolea Taarifa tar 20 April 2020. Mchanganuo wa wagonjwa wapya 30 ni kama ifuatavyo: Dar es salaam (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani (2), Kagera (1), Dodoma (2), Manyara (1) na Morogoro (1) 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post