DK. NDUGULILE ATOA UFAFANUZI KUHUSU BARAKOA NA MATUMIZI YAKE


UFAFANUZI KUHUSU BARAKOA NA MATUMIZI YAKE

Kuna clip inazunguka mitandaoni nikiongelea kuhusu barakoa za kitambaa. Napenda kutoa ufafanuzi ufuatavyo:


1. Barakoa za N95 zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa Covid-19. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini.

2. Barakoa za upasuaji (surgical masks) hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawana direct contact na wagonjwa. Barakoa hizi pia zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6. Barakoa hizi hazipaswi kuvaliwa kutwa nzima na kurudia matumizi (re-use). 

Aidha, kumekuwa na sintofahamu kuhusu namna ya uvaaji wa barakoa za upasuaji. Barakoa hizi zinapaswa kuvaliwa kama ifuatavyo:

(a). Upande wenye rangi (blue, kijani, zambarau nk) unapaswa kuwa nje.

(b). Upande wenye chuma unapaswa kuwa juu.

3. Barakoa za kitambaa (cloth masks) hazina ubora wa kinga kama N-95 au  surgical masks, lakini zinaweza kutumika kupunguza uwezekano wa maambukizi toka kwa mtu mmoja kwenda mwingine majumbani na sehemu za mikusanyiko.  

Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:

1. Kutumia vitambaa vya pamba.

2. Kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo.

3. Kuwa na  barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara.

4. Barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi.

NI MUHIMU KUKUMBUKA KUWA BARAKOA SIO MBADALA WA KUNAWA MIKONO NA KUZINGATIA UMBALI KATI YA MTU NA MTU (SOCIAL DISTANCING) BALI NI NYONGEZA YA HATUA HIZI. 

Aidha, tuhakikishe barakoa zilizotumika hazitupwi ovyo na badala yale zichomwe moto ili kuepuka kuokotwa na kutumiwa 
na watu wengine.

 Vile vile, watu hawapaswi kuazimana barakoa iliyokwisha kutumika. Kila mtu awe na yake.

Mwisho, tuendelee kuzingatia maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Wizara ya Afya kuhusu hatua mbali mbali za kujikinga na ugonjwa huu.

Dkt Faustine Ndugulile (Mb)
19.04.2020

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527