WATU 354 CORONA WAPATA MAAMBUKIZI YA CORONA NDANI YA MASAA 24 AFRIKA KUSINI....WALIOMBUKIZWA HADI SASA NI 5350


Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Afrika Kusini imefika watu 5,350 baada ya visa vipya 354 kuthibitishwa, huku idadi vifo ikifikia watu 103.Taarifa kutoka wizara ya afya imesema visa vipya 354 ni vya juu kuwahi kuripotiwa  nchini humo chini ya kipindi cha saa 24.

Takriban wiki sita zimepita tangu kisa cha kwanza cha Covid 19 kuripotiwa nchini Afrika Kusini, na idadi ya maambukizi imekuwa ikiongezeka .

Hivi karibuniAfrika Kusini ilichukuwa mikakati mipya kupambana dhidi ya Corona katika magereza mbalimbali nchini humo, baada ya wafungwa 59 na wafanyakazi wa gereza 29 kuthibitishwa kuambukizwa katika kipindi cha majuma mawili.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post