Picha : MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MKOA WA SHINYANGA RAHA MTUPU...SHUHUDIA HAPA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) ameongoza Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Akizungumza katika maadhimisho hayo yenye Kauli mbiu “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”, Mhe. Azza aliwataka wanawake kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 wachague viongozi waadilifu,wawajibikaji na wenye nia ya kuleta mabadiliko. 

“Nina imani kubwa wanawake mtajitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika Uchaguzi Mkuu”,alisema  Mhe. Azza. 

“ Naomba niwakumbushe kuwa mwanamke ni fursa katika uchumi wa kaya apewe kipaumbele katika maamuzi ya familia na jamii. Wakati ni sasa chukua hatua,mwanamke simama chukua nafasi kwa maendeleo endelevu ya Tanzania ya sasa nay a baadae”,alisema Mhe. Azza. 

Alisema licha ya serikali kuendelea na mikakati mbalimbali ya kumuinua mwanamke lakini bado eneo la mila na desturi gandamizi,potofu na zenye madhara kuwa ni kikwazo cha kufikia maendeleo ya 50 kwa 50 hususani katika uchumi wa viwanda. 

Mbunge huyo,alitumia fursa hiyo kuwapongeza wanafunzi na walimu wa shule ya Msingi Ilobi iliyopo wilayani Kishapu kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kuhitimu darasa la saba mwaka 2019 na kuuletea mkoa wa Shinyanga heshima ambapo kati ya wanafunzi bora wa kike, watano walitoka katika shule ya Ilobi. 

“Shule ya msingi Ilobi wameuletea heshima kubwa mkoa wa Shinyanga. Wanafunzi na walimu wa shuli hii wanahitaji kupewa motisha na shule zingine zikajifunze pale wanafanya nini. Binafsi niliwapatia Kompyuta na Printer yake kama motisha kwao”,alisema Azza. 

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani mkoa wa Shinyanga yalianza kwa maandamano ya wadau wa haki za wanawake, ambapo Wanawake wameonesha ujuzi wao na vipaji kwa kuendesha magari, mitambo mikubwa ya kutengeneza miundombinu ya barabara pamoja na gwaride ya Wanawake askari lengo ni kuwatia motisha ya kuachana na mila na desturi za ukandamizaji wa Wanawake na Mtoto wa kike. 

Mgeni rasmi Azza Hilal pia alikabidhi taulo laini za kike zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba 2020. 

Matukio mengine ni pamoja na Mhe.Azza Kuzindua Timu ya Wanawake mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga ‘Shinyanga Super Queen’, kukabidhi Vifaa vya kazi’ Aproni’ kwa Mama Lishe 300 na shilingi 500,000/= kwa mwanamke mwenye ulemavu. 

Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga,Tedson Ngwale aliwataka wadau waliofanikisha maadhimisho ya siku ya wanawake mkoa wa Shinyanga kuwa ni pamoja na shirika la World Vision, VSO,CUAMM,Thubutu Africa Initiatives,Rafiki SDO, Life Water International ,Pathfinder,USAID Tulonge Afya,RUDI,YADEE,TANESCO,IBA,TANROADS,TEMESA,ICS,AGAPE,VODACOM,Benki ya CRDB na Kampuni ya Jambo Food Products Ltd.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, James Bwana akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wadau wa haki za wanawake wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Wa pili kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na viongozi mbalimbali wakiwasili kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikagua kikundi cha wanawake/vijana wa kike wanaojihusisha na masuala ya ujenzi wa nyumba.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika banda la Benki ya CRDB.
Afisa wa Benki ya CRDB akimuelezea Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa katika banda la USAID Tulonge Afya.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na viongozi mbalimbali wakipokea maandamano ya wadau wa haki za wanawake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Askari polisi wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Askari polisi wanawake wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye maandamano wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga.
Wanawake wakiwa katika maandamano.
Wanawake wakiwa kwenye maandamano.
Wanawake wanaoendesha magari na mitambo ya kuchonga barabara wakiwa kwenye maandamano.
Wanawake wanaoendesha magari na mitambo ya kuchonga barabara wakiwa kwenye maandamano.
Maandamano yanaendelea.
Wadau wakiendelea na maandamano.
World Vision wakiwa kwenye maandamano.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Maandamano yanaendelea.
Wadau wakiwa kwenye eneo la tukio.

Burudani ya ngoma ikiendelea.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) na viongozi wengine wakielekea katika uwanja wa Iselamagazi kwa ajili ya Kuzindua Rasmi Timu ya Wanawake ya mpira wa miguu ya 'Shinyanga Super Queen'.
Wachezaji wa timu za wanawake ' Ngokolo Secondary' kulia na Shinyanga Super Queen wakiwa uwanjani kabla ya kuanza mchezo wa Kuzindua Rasmi Timu ya Wanawake ya mpira wa miguu ya 'Shinyanga Super Queen'.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Wanawake mkoa wa Shinyanga ' Shinyanga Super Queen'
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akizindua  Timu ya Wanawake mkoa wa Shinyanga ' Shinyanga Super Queen' kwa kurusha mpira.
Mchezo kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakifuatilia mtanange kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakifuatilia mtanange kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakifuatilia mtanange kati ya Shinyanga Super Queen' na Ngokolo ukiendelea ambapo dakika 30 za mchezo zilimalizika kwa timu ya Shinyanga Super Queen Kuichapa Ngokolo Secondary bao 3 -0.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maafisa wa Shirika la World Vision wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya mbuzi wawili kwa Mariam Amos mkazi wa Lyabusalu kwa kuwa mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kuzunguka uwanja wa mpira mara nne.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi zawadi ya mbuzi wawili kwa Eunice Emmanuel mkazi wa Mwambasha kwa kuwa mshindi wa pili mbio za baiskeli kuzunguka uwanja wa mpira mara nne.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akicheza muziki na wanawake wakati nyimbo kuhusu wanawake zikipigwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Wanawake wakicheza muziki wakati nyimbo kuhusu wanawake zikipigwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha shilingi 500,000/= zilizotolewa na zilizotolewa na Kampuni ya Utengenezaji na Usambazaji wa Vinywaji baridi ‘Jambo Food Products Limited’ kwa ajili ya  Mwanamke mwenye ulemavu Bi.Happiness Kwigema anayejishughulisha na biashara ya pipi na sabuni za kufulia Mjini Shinyanga. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited’,Esme Salum.
Wanafunzi na wadau wakiwa eneo la tukio.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya Mama Lishe katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga baada ya kuwakabidhi vifaa vya kazi 'Aproni'.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya kumbukumbu na Mama Lishe na Wakurugenzi/Wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri za wilaya 6 za mkoa wa Shinyanga waliopokea  Aproni na watakwenda kuzigawa kwa Mama Lishe waliopo katika halmashauri zao.
Wanafunzi wakiwa kwenye eneo la tukio.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akielezea namna alivyoshirikiana na wadau mbalimbali kufanikisha kupatikana kwa taulo laini za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020 zenye thamani ya shilingi Milioni 7.7. Kushoto ni sehemu ya maboksi 66 yenye taulo hizo laini za kike.
Meneja Biashara Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddi akionesha risti ya malipo ya fedha iliyotolewa na Benki ya CRDB na kuchangia kufanikisha kupatikana kwa taulo laini za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wanaotarajia kumaliza elimu ya darasa la saba mwaka 2020 zenye thamani ya shilingi Milioni 7.7 zilizotolewa na wadau mbalimbali mkoa wa Shinyanga waliomuunga Mkono Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga.  Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Food Products Limited, Esme Salum.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa ameshikilia Taulo laini za kike na wanafunzi wanaosoma darasa la saba katika shule mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) akipiga picha ya pamoja na baadhi ya wadau mbalimbali waliofanikisha kupatikana kwa  Taulo laini za kike ‘ Pedi’ zenye thamani ya shilingi milioni 7.7 kwa ajili ya wanafunzi 780 wanaotarajia kuhitimu elimu ya darasa la saba mwaka 2020 kutoka shule 30 mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa eneo la tukio.
Maafisa kutoka Shirika la World Vision wakionesha ishara ya usawa la Kijinsia kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani mkoa wa Shinyanga.
Mc Mzungu Mweusi (kushoto) na MC Elipendo John wakiendelea kutoa maelekezo mbalimbali kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Wadau wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mkoa wa Shinyanga ambayo yamefanyika Machi 8,2020 katika kata ya Iselamagazi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527