WAJUMBE WATATU YANGA WAJIUZULU, WAWILI WASIMAMISHWA

Wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji Yanga wametangaza kujiuzulu nafasi zote walizokuwa nazo , huku wengine wawili wakisimamishwa kwa utovu wa nidhamu, ikiwa siku chache tangu Kampuni ya GSM kutishia kusitisha huduma zake klabuni.


Waliotangaza kujiuzulu na maamuzi yao kukubaliwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ni Rodgers Gumbo, Said Kambi na Shija Richard, huku waliosimamishwa kwa muda usiojulikana ni pamoja na vigogo wa Kamati ya Usajili, Frank Kamugisha na Salim Rupia.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post