Picha : FUSO YAGONGANA NA GARI NDOGO ROUND ABOUT SHINYANGA MJINI…SPIDI KALI YATAJWA

Kumetokea ajali katika Mzunguko wa Barabara’ Round About’ ya Japanese Corner Mjini Shinyanga ambapo Fuso lenye Namba za usajili T609 COL kugongana na gari dogo aina ya IST lenye namba za usajili T435 DGL leo Ijumaa Machi 27,2020 majira ya moja na nusu usiku.Mashuhuda wa tukio waliozungumza na Malunde 1 blog wamesema chanzo ni mwendo kasi wa dereva wa lori hilo ambaye baada ya kufika katika Round About hiyo gari lilimshinda na kugonga gari ndogo na kupinduka katika eneo.“Hili Lori lilikuwa katika speed kali likitokea barabara ya Lubaga na dereva alipofika katika Round About alijaribu kufunga breki lakini kutokana na mwendo kasi aliokuwa nao gari lilimshinda na kupinduka mara kadhaa na kugonga gari ndogo”,wamesema mashuhuda.

“Ndani ya lori kulikuwa na wanaume watatu na kwenye gari ndogo kulikuwa na mwanamke,wote wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu”,wameongeza.

Malunde 1 blog imeshuhudia miundo mbinu ya Round About hiyo ikiwa imeharibika kutokana na ajali hiyo huku askari wa usalama barabarani wakiwa eneo la tukio kuongoza magari kuepusha foleni na kuondoa wananchi waliofurika katika eneo hilo kushuhudia ajali hiyo.

Tutakutaarifu zaidi baada ya kuzungumza na Mamlaka zinazohusika ikiwemo jeshi la polisi kwa  taarifa zaidi kuhusu ajali hiyo..Endelea kutembelea Malunde 1 blog.
Muonekano wa Lori baada ya kupata ajali katika eneo la Round About eneo la Japanese Corner Mjini Shinyanga . Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mashuhuda wakiwa eneo la tukio
Muonekano wa lori baada ya ajali
Muonekano wa gari ndogo baada ya ajali Round About Shinyanga Mjini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post