Tanzia: MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA ILALA DK MAKONGORO MAHANGA AFARIKI DUNIA



 
 Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Ilala, Dk Milton Makongoro Mahanga amefariki dunia  leo Jumatatu Machi 23, 2020katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa Chadema Kanda ya Pwani, Hemed Ally amesema wamepata taarifa za msiba huo.

“Ni kweli taarifa hizo tumezipata kupitia katibu wa Chadema wa Mkoa wa Ilala maana yeye ndiye alikuwa anafanya naye kazi kwa ukaribu,” amesema.

“Ilikuwa twende tukamuone leo na taarifa zote zilikuwa zinapitia kwa katibu wake wa mkoa wa Ilala wa chama, sasa asubuhi alipofanya mawasiliano na mke wake akamueleza kuwa Dk Makongoro amefariki dunia,” amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527