AJALI YA TRENI YAUA WATUMISHI WATANO TANZANIA


Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania -TEC unatangaza taarifa za Vifo vya watumishi 5 wa TRC.Vifo hivyo vimesababishwa na ajali ya Treni ya uokoaji kugongana na Kiberenge No.HDT-3 katika maeneo yaliyopo kati ya stesheni za Mwakinyumbi na Gendagenda tarehe 22.3.2020.

Eneo hili lipo katika Reli inayotoka Ruvu Junction  mpaka Mruanzi Junction.
Watumishi wa TRC walikua sita, Watumishi wanne wamefariki pale pale  katika eneo la ajari na majeruhi wawili walifikishwa katika Hospitali  ya Wilaya ya(magunga) Korogwe kwa huduma za Kitabibu.

Mpaka  ilipofikia saa tano usiku (23:00) tarehe 22.3.2020 majeruhi mmoja alifariki na kufikia jumla ya  watumishi wa TRC watano wamefariki.

Watumishi hao ni :
1.Ramadhani Gumbo-DTM Tanga
2.Eng.Fabiola Moshi DME DSM
3.Joseph Komba - ATM DSM
4.Philip Kajuna -Safety Technical
5.George Urio - Dereva wa trolley

Mpaka sasa majeruhi mmoja anaendelea na matibabu ni Guard wa treni Elizabeth Bona.

Poleni sana familia ya Reli kwa tukio hili la kusikitisha sana.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusu maandalizi ya kuhifadhi miili ya wapendwa wetu.

Aidha uchunguzi wa kujumuisha taasisi zingine utafanywa kubaini chanzo cha ajali hii mbaya.

Bwana ametwaa na Bwana ametoa, Jina lake lihidimiwe🙏🙏


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527