TANZANIA KUUZA MAKONTENA 200 YA MAHARAGE NCHINI UBELGIJI...CHANGAMKIA HIYO FURSA!!


Ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji umepata soko kubwa la maharage machanga ya kijani yanayojulikana kama haricots vertz(green thin beans) nchini Ubelgiji. 


Soko hilo limepatikana baada ya Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga kufanya mazungumzo  na uongozi wa juu wa kampuni ya CBG-Charlier-Brabo Group inayonunua maharage hayo kutoka sehemu mbalimbali duniani na kuyauza katika supermarkets kubwa za Carrefour, Delhaize na Aldi za nchini Ubelgiji, Luxembourg na nchi nyingine za Ulaya.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika tarehe 3 Machi 2020, kampuni hiyo ipo tayari kununua containers kati ya 180-200 za maharage hayo kila mwaka kutoka Tanzania.

Kupatikana kwa soko la maharage hayo nchini Ubelgiji ni habari njema kwa wakulima wa Tanzania na wafanyabiashara wa mazao ya kilimo hususan wa aina hiyo ya maharage ambayo tayari Tanzania inayauza nchini Uholanzi.

Kampuni hiyo pia imeonesha utayari wa kununua aina nyingine ya maharage ijulikanayo kama red kidney beans na chickpea kwa kiwango cha containers 8 kila mwaka katika hatua za mwanzo.

Ubalozi wa Tanzania unatoa wito kwa Watanzania kuchangamkia upatikanaji wa soko hilo jipya nchini Ubelgiji kwa kuwasiliana na kampuni hiyo kupitia tovuti yao ya www.cbg.be au kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa maelekezo zaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post