KONGAMANO LA KILIMO LASITISHWA KUEPUKA MAAMBUKIZI YA CORONA

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Japhet N. Hasunga (Mb) amesitisha kongamano la vijana katika kilimo lililokuwa limepangwa kufanyika Jumanne tarehe 17 Machi 2020 katika ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Agizo hili ametolewa  kufuatia maelekezo yaliyotolewa na Serikali ya kuchukua tahadhari ya mikusanyiko ya watu wengi kuepusha hatari ya kusambaa kwa maambukizo ya virusi vya Corona nchini.

Wizara ya Kilimo inawataarifu wadau wote wa sekta ya kilimo na vijana waliopanga kushiriki kongamano la kujadili fursa za kilimo,mifugo na uvuvi kwa kanda ya Dar es Salaam iliyokuwa ikihusisha mikoa ya Dar es Salaam,Pwani,Morogoro,Lindi na Mtwara kusitisha kuhudhuria kongamano hilo hadi watakapotaarifiwa baadaye.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametoa rai kwa Watanzania kuchukua tahadhali na vihatarishi vinavyoweza kusababisha maambukizi ya Corona kwa kuepuka mikusanyiko ya watu wengi isiyo ya lazima alisema Waziri Hasunga.

Mheshimiwa Waziri Hasunga amewataka wakulima na vijana wote nchini kuendelea kuchukua hatua za tahadhali kwa kuzingatia maelekezo ya Wizara ya Afya yaliyotolewa ili kuthibiti maambukizo ya virusi hivi hatari vya Corona hapa nchini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527