RAIS MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI LEO CHAMWINO – DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino. Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Chamwino Dodoma. Machi 24, 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya Pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa,Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino – Dodoma. Machi 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu akitoka nje ya ukumbi wa Baraza la Mawaziri mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu Chamwino – Dodoma. Machi 24, 2020.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, ajira Vijana na Walemavu Mhe. Stella Ikupa  na viongozi wengine mara baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino – Dodoma. Machi 24, 2020.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipima joto la mwili kabla ya kuingia katika ukumbi wa Baraza la Mawaziri kuongoza kikao cha Baraza hilo. Kikao hicho kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Mawaziri wote, Manaibu Mawaziri pamoja na Viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Chamwino Dodoma. Machi 24, 2020.

PICHA NA IKULU


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527