RC MAKONDA AAGIZA KUPULIZWA DAWA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM ILI KUKABILIANA NA CORONA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kupulizwa dawa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kuanzia kesho, ili kuua vijidudu vinavyoeneza magonjwa vikiwemo virusi vya corona ambavyo vimeathiri watu kumi na mbili nchini hadi sasa.

Makonda ameyasema hayo alipotembelea kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, lengo likiwa ni kujiridhisha kama watoa huduma katika kituo hicho wanachukua hatua za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Amewaeleza wasafiri waliokuwepo kituoni hapo kuwa virusi vya corona ni hatari, hivyo wachukue tahadhari kwa kujikinga wao wenyewe pamoja na kuwakinga wengine.

Aidha, amewataka wakazi wa mkoa huo wa Dar es salaam kutoa taarifa mapema endapo watabaini kuwepo kwa mtu mwenye dalili zinazofanana na za mgonjwa wa homa ya corona, na kwa mtu anayehisi kuwa na dalili za homa hiyo atoe taarifa ili aweze kupatiwa huduma zinazostahili.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527