POLISI WASEMA MZEE MANGULA ALIPEWA SUMU


Kamanda wa Polisi Kanda Malumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amesema kuwa baada ya uchunguzi kufanyika imebainika kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula, aliwekewa sumu ijapokuwa bado haijajulikana aliwekewa kwa njia ipi.

Akizungumza leo Machi 9, 2020 na Waandishi wa Habari, Kamanda Mambosasa amesema kuwa taarifa hizo walizipata Februari 28,2020, hii ni baada ya Mzee Mangula kudondoka ghafla katika ofisi ndogo zilizopo Lumumba mara baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa, iliyokuwa ikijadili mambo mbalimbali ikiwemo adhabu kwa wanachama wake watatu.

"Katika taarifa hiyo tulielezwa kwamba, Mzee Mangula alipelekwa Muhimbili na kulazwa ICU, Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama limebaini kwamba ndani ya mwili wa Mzee Mangula ulipatikana na sumu, kwa yeyote atakayebainika kupanga, awe ndani ya CCM, mwanafamilia ama Serikalini hatua kali zitachukuliwa dhidi yake " amesema Kamanda Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa upelelezi kuhusu namna ambavyo sumu hiyo iliingia mwilini bado unaendelea, na Jeshi hilo halitasta kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika na uhalifu huo


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post