POLISI NCHINI KENYA YAUSAKA MTANDAO WA WATU 85 UNAOHUSISHWA NA MGONJWA WA CORONA ALIYETOROKA HOSPITALI

Serikali Nchini Kenya inawasaka watu 85 wanaohofiwa kuambukizwa virusi vya corona baada ya kuambatana na mgonjwa wa virusi hivyo katika hospitali ya Mbagathi. Mgonjwa huyo anasemekana kutoroka katika wodi iliyotengewa wagonjwa wa Corona katika hospitali hiyo ila alikamatwa baadaye na maafisa wa ulinzi. 

Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi nchini, Seth Panyako alithibitisha kisa hicho kupitia kwenye hotuba yake na wanahabari Jumatano, Machi 18.

 " Kuna mgonjwa aliyepelekwa katika hospitali ya Mbagathi akiwa na virusi hivyo, aliondoka hospitalini humo bila kupewa ruhusa lakini maafisa wa ulinzi walifanikiwa kumkamata . Kwa sasa tunawasaka wagonjwa wengine 85 waliotangamana naye". Panyako alisema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post