BENKI KUU YA TANZANIA YATOA UFAFANUZI KUHUSU NOTI ZA TANZANIA NA VIRUSI VYA CORONA


Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutarifu umma kwamba noti zetu zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia kwenye noti. 


Hata hivyo, kwa kuwa noti hizo zinapita katika mikono mingi, tunawashauri wananchi kuzingatia miongozo mbalimbali inayotolewa na mamlaka zenye dhamana ya afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizers). Kufanya hivyo kutasaidia kuua vimelea kwenye mikono.

Aidha, tunawashauri wananchi kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama vile simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti.

Kama ilivyotangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), Ugonjwa wa Corona ni tishio duniani kote na tayari umeingia nchini tangu Jumatatu Machi 16, 2020 kwa mgonjwa wa kwanza kupatikana mkoani Arusha na wagonjwa wengine wawili mmoja huko Zanzibar na mwingine jijini Dar es Salaam ambao walitangazwa jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, na hivyo kufanya jumla ya wagonjwa wa Corona (COVID-19) hapa nchini kufikia watatu.

Tunawasihi wananchi katika kipindi hiki ambacho taifa liko katika mapambano dhidi ya COVID-19 kuzipuuza taarifa zinazozagaa mitandaoni ambazo hazina vyanzo vya uhakika, zinazozihusisha noti zetu na usambazaji wa virusi vya corona



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527