Kesi ya Tundu Lissu Yakwama Tena

Kesi inayomkabili aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake imeshindwa kuendelea baada ya Upande wa Mashtaka kushindwa kuwasilisha jalada la kesi hiyo

Mahakama hiyo jana ilitarajia kusikiliza maombi yaliyowasilishwa na wadhamini wa mshitakiwa huyo wakiomba mahakama kutoa hati ya kumkamata mshitakiwa huyo kwa kuwa wao wameshindwa.

Wakili wa Serikali, Ester Martin alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa mwendesha mashitaka anayesikiliza shauri hilo hayupo hivyo anaomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusikilizwa.

Baada ya Upande wa mashitaka kuwasilisha hoja hiyo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 23, 2020 kwa sababu ya Upande wa Mashitka umeshindwa kuwasilisha jalada la kesi hiyo mahakamani hapo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post