Picha : MAOMBI YA WANAWAKE NA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA SHINYANGA, DC MBONEKO ATAKA WAJITOKEZE KUGOMBEA UONGOZI UCHAGUZI MKUUMaombezi ya wanawake na watoto duniani katika manispaa ya Shinyanga yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake kutoka Makanisa ya Kiinjili Tanzania (CCT ) Shinyanga mjini, yamefanyika leo Ijumaa Machi 6,2020 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwaka huu.

Maombezi ya wanawake duniani katika manispaa ya Shinyanga  kwenye kanisa la AICT Ngokolo na kuhudhuriwa na wanawake kutoka kwenye makanisa mbalimbali ya Kikristo ya Shinyanga, ambapo mgeni Rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko.

Akizungumza kwenye maombezi hayo Mboneko, amewataka wanawake katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais, wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, kama walivyojitokea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana.

“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo naomba wanawake wenzangu mjitokeze kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi huu, kama mlivyofanya kwenye uchaguzi uliopita wa Serikali za mitaa ambapo mlijitokeza wengi kweli na sasa tuna viongozi wanawake kwenye vitongoji, mitaa na vijiji,”alisema Mboneko.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa viongozi wa dini kwenda kutoa mahubiri ya neno la Mungu hasa maeneo ya vijijini, ili wananchi wamuamini Mungu na kuacha kwenda kutibiwa kwa waganga wa kienyeji, ambao wamekuwa wakipiga ramli chonganishi na kusababisha mauaji ya watu wasio na hatia hususani wanawake.

Naye Katibu wa Umoja wa Wanawake kutoka Makanisa ya Kiinjili Tanzania CCT Manispaa ya Shinyanga Teckla Mongela, akisoma risala kwenye maombi hayo, aliiomba Serikali kumaliza tatizo la mauaji ya wanawake na kutolewa viungo vyao, changamoto ambayo imekuwa ikiwakosesha amani.

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Julia Selestine kutoka Buzuruga Jijini Mwanza, amewataka wanawake kuacha matukio ya ukatili majumbani mwao kwa kunyanyasa wanaume, bali wawe watii katika ndoa zao ili kuepusha vifo vya ghafla kwa waume zao na kubaki wajane.

Amesema sasa hivi wanawake wamegeuka kuwa wanyanyasaji kwa waume zao, hasa pale wanapopata fedha za vikoba na kujiona kichwa katika familia, na kuanza kutowatii wanaume na hata kuwanyima unyumba, hali ambayo imekuwa ikisababisha wanaume kufariki kwa mshituko wa moyo sababu ya kuhifadhi mambo hayo moyoni.


TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye siku ya maombezi ya wanawake duniani katika manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika kwenye kanisa la AICT Ngokolo leo Jumamosi Machi 6,2020. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye siku ya maombi  ya wanawake duniani katika manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika kwenye kanisa la AICT Ngokolo na kuwataka wanawake wajitokeze kugombea uongozi kwenye uchaguzi mkuu.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko katikati akipokea maandamano ya umoja wa wanawake kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo Shinyanga mjini, katika kanisa la AICT Ngokolo Shinyanga mjini kwa ajili ya kuongoza maombezi ya wanawake duniani, ambapo maombezi ya watoto yatafanyika Machi 14 mwaka huu, kulia ni mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kiinjili manispaa ya Shinyanga Marysiana Makundi na kushoto ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini mashariki ya Ziwa Victoria, Dk. Emmanuel Joseph Makala.

Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Julia Selestine kutoka Buzuruga Jijini Mwanza, akizungumza kwenye siku ya maombezi ya wanawake duniani yaliyofanyika manispaa ya Shinyanga kwenye Kanisa la Ngokolo.

Katibu wa Umoja wa Wanawake kutoka makanisa ya Kiinjili Tanzania CCT Manispaa ya Shinyanga Teckla Mongela, akisoma risala kwenye siku ya maombezi duniani yaliyofanyika Ngokolo Shinyanga mjini kwenye kanisa la AICT Ngokolo.

Wanawake kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo Shinyanga mjini wakiwa kwenye ibada ya siku ya maombezi ya wanawake duniani yaliyofanyika kwenye kanisa la AICT Ngokolo.

Ibada ya maombezi ya wanawake ikiendelea.

Ibada ya maombezi ya wanawake ikiendelea.

Ibada ya maombezi ya wanawake ikiendelea.

Ibada ya maombezi ya wanawake ikiendelea.

Ibada ya maombezi ya wanawake ikiendelea.

Maaskofu kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo Shinyanga mjini wakiwa kwenye ibada hiyo ya maombezi ya wanawake duniani, yaliyofanyika Shinyanga mjini kwenye kanisa la AICT Ngokolo.

Kwaya zikiimba nyimbo kwenye siku ya maombezi hayo ya wanawake.

Nyimbo zikiendelea kuimbwa.

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post