CHADEMA WASITISHA MIKUTANO YA HADHARA KUKABILIANA NA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, March 23, 2020

CHADEMA WASITISHA MIKUTANO YA HADHARA KUKABILIANA NA CORONA

  Malunde       Monday, March 23, 2020
Na Faustine Gimu

Chama  cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha tamko lake la kufanya mikutano ya hadhara kote nchini kutokana na ugonjwa wa Corona.


Mikutano hiyo iliyotangazwa kufanyika kuanzia April 04 mwaka huu imesitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho  Mh.Freeman Mbowe hii leo jijini Dodoma.

Akizungumza leo Machi 23, 2020, Jijini Dodoma, Mbowe amesema kuwa wakati anatoa kauli yake ya kutangaza uwepo wa mikutano ya hadhara kwa nchi nzima, Serikali haikuwa imetangaza uwepo wa mgonjwa yeyote wa Virusi vya Corona na kwamba wataendelea na mikutano yao pale ambapo hali ya ugonjwa huo itakuwa imetengemaa.

Aidha Mbowe ameiomba Serikali ione ipo haja ya kufunga mipaka yake yote ili kuhakikisha hakuna mgeni yoyote anayeingia nchini kutoka kwenye Mataifa yaliyoathirika na Virusi vya Corona.

Wakati huo huo Chama hicho kimetoa salamau za pole kwa familia kufatia kifo cha aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa kazi na ajira kabla ya kuhama Chama cha Mapinduzi na kuhamia CHADEMA ambako alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Ilala Dkt.Makongoro Mahanga


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post