MBOWE NA VIGOGO WENGINE CHADEMA WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 350 AU KWENDA JELA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake kulipa faini ya Sh.Mil 350 ama kwenda jela miezi 5 baada ya kutiwa hatiani kwenye makosa 12 ikiwemo la kufanya maandamano.

Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa 4, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 11 jioni, imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi 23 baina ya utetezi na Serikali.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema amewatia hatiani washitakiwa katika mashitaka 12 kati ya 13.

Kosa ambalo hawajatiwa nalo hatiani ni kosa la kwanza ambalo ni kufanya mkusanyiko usio halali.

“Mashitaka waliyotiwa hatiani ni mabaya katika jamii ukizingatia wao ni viongozi na walitakiwa kuwa mstari wa mbele katika utii wa sheria, hivyo mahakama inaona kuwa wanastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine watakaofanya makosa kama ha

“Natoa adhabu kali kwa kuzingatia hoja ya kuwa washitakiwa ni wakosaji wa kwanza na wanatakiwa kupewa huruma na ukizingatia wengine walishakaa mahabusu, hivyo kukaa kwao ndani ni adhabu tosha kwa mantiki hiyo nawaepusha na adhabu ya vifungo kwa washitakiwa wote,” shangwe zikapigwa.

Katika adhabu hiyo, Mbowe amehukumiwa kulipa Sh.Mil 70, Halima Mdee Sh.Mil 40, Dr.Mashinji kulipa Sh.Mil 30, John Heche Sh.Mil 40, Msigwa Sh.Mil 40, Bulaya Sh.Mil 40, Mnyika Sh.Mil 30, Salum Mwalimu Sh.Mil 30 na Ester Matiko Sh.Mil30.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post