JESHI LA SYRIA LADHIBITI TENA MJI WA KIMKAKATI WA SARAQEB...UTURUKI YAITISHIA ULAYA, URUSI YATIA NENO


Vikosi vya utawala vya Syria vinadhibiti tena Saraqeb, tangu Jumatatu Machi 2. Saraqeb ni eneo la kimkakati nchini Syria. 


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, anatarajiwa kuzuru Urusi, Alhamisi Machi 5.

Recep Tayyip Erdogan anatarajia kupata mkataba wa kusitisha mapigano kutoka kwa mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. 

Recep Tayyip Erdogan anaendelea kuongeza shinikizo na kutishia kufungua mipaka yake kuwaruhusu wahamiaji na wakimbizi kutoka Syria wanaotafuta hifadhi katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Jeshi la Syria liliingia Saraqeb Jumatatu wiki hii, eneo ambalo linapatikana kwenye karibu na barabara mbili muhimu, Kusini Mashariki mwa mji wa Idleb.

Saraqeb imedhibitiwa mara kadhaa katika wiki za hivi karibuni na vikosi vya serikali, na baadaye makundi ya waasi kwa msaada wa Uturuki wiki iliyopita na sasa hivi imerudi kudhibitiwa na vikosi vya serikali ya Bashar Al Assad.

Urusi imetangaza kwamba vitengo vya Askari jeshi la Urusi vimepelekwa Saraqeb, hali ambayo inaonyesha kuwa sasa Moscow inadhibiti eneo hilo.

Kulingana na shirika la Haki za binadamu nchini Syria, OSDH, askari zaidi ya 90 wa serikali wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Uturuki tangu siku ya Ijumaa pamoja na wapiganaji 10 wa Hezbollah.

Mkutano kati ya marais wa Urusi na Uturuki umepangwa kufanyika Alhamisi, Machi 5 huko Moscow. Recep Tayyip Erdogan amesema atataka vita visitishwe nchini Syria.

Vladimir Putin na Recep Tayyip Erdogan wanaunga mkono pande hasimu nchini Syria.

Credit-RF/VOA


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post