VIJANA WA SKAUTI WATAKIWA KUWA MABALOZI WAZURI KUTOA ELIMU YA MADHARA YA RUSHWA

Na Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Vijana  wa Skauti hapa nchini wametakiwa kuwa Mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwa Umma  juu ya madhara ya rushwa.


Rai hiyo imetolewa jana Machi,2,2020  jijini Dodoma na Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala bora Kapteini Mstaafu George Mkuchika wakati   wa uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa mapambano dhidi ya rushwa kwa kuwatumia vijana wa skauti nchini.

Kaptein Mkuchika akizungumza kwa niaba ya mgeni Rasmi katika uzinduzi huo,makamu wa Rais  Samia Suluhu,amesema rushwa inadhoofisha haki hivyo ni jukumu la kila mmoja katika mapambano hayo.

“Mapambano dhidi ya  rushwa ni jukumu letu sote tushiriki mapambano dhidi ya rushwa ,ninyi vijana wa skauti mkawe mabalozi wazuri katika kutoa elimu kwa umma”amesema.

Kwa upande wake ,Rais Mstaafu wa awamu  ya pili Ally Hassan Mwinyi ameitaka jamii kukitumia vyema Kiswahili fasaha  katika kutoa elimu juu ya madhara ya rushwa kwani rushwa ni adui wa haki.

Mskauti mkuu Tanzania Mwamtumu Mahiza amesema zaidi ya  wanafunzi milioni 10  na laki 6 wa  shule za msingi na sekondari hapa nchini  wameandaliwa kusambaza  elimu ya rushwa   ambapo matarajio ni kufikia watu milioni 40 kupata elimu hiyo.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU nchini Brigedia Jen John Mbungo  amesema Mpango wa Uzinduzi wa mkakati wa kitaifa wa mapambano dhidi ya rushwa kwa kutumia vijana wa skauti nchini  utasaidia kuongeza vijana  maaskari wa mapambano hayo katika jamii.

Waziri wa katiba na sheria Dkt.Augustine Mahiga amesema rushwa ni maradhi ambukizi na isipokomeshwa inaiva  hivyo  yake imeendelea kusimamia sheria kuhusiana na kuwabana  wala rushwa hususan kuanzisha mahakama maalum ya kupambana na Mafisadi.

Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako amesema vijana hususan Shuleni wanatakiwa kuwa chachu na kufanya mabadiliko katika mapambano dhidi ya rushwa ambapo amesema wizara yake itashirikiana na TAKUKURU pamoja na Skauti Tanzania katika  kuwasimamia vijana katika mapambano hayo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post