FAINALI YA REDE KUPIGWA LEO MKWAKWANI TANGA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertaiment Nasoro Makau ambao ndio waandaaji wa Mashindano ya Rede Jijini Tanga akizungumza na waandishi wa habari kuelekea Fainali ya Mashindano hayo kushoto ni
Mratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango kulia ni Msimamizi wa Waamuzi Magdalena Liwemba
 Mratibu wa Mashindano hayo Zaituni Mango akisisitiza jambo kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Brothers Intertaiment Nasoro Makau ambao ndio waandaaji wa Mashindano ya Rede Jijini Tanga na Msimamizi wa Waamuzi Magdalena Liwemba
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali

FAINALI ya Mashindano ya Rede itafanyika leo kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga huku ushindani mkubwa ukitarajiwa kujitokeza kutokana na timu zilizoingia kwenye hatua hiyo.

Mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yameandaliwa na Kampuni ya Five Brothers Intertaiment kupitia Mkurugenzi wake Nassoro Makau.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuekelea fainali hiyo Makau alisema kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa na timu ambazo zitachuana zimeanza kujiandaa vema.

Alisema kwamba wamejikita kuhakikisha michezo yote ya zamani wanairudisha ikiwemo Rede ambao kwa sasa mashindano hayo ni msimu wanne ambao umekuwa mchezo mkubwa na kuweza kutambulika na kupata mialiko mbalimbali hata kwa mikoa ya jirani.

Aidha alisema malengo yao na kuhakikisha mchezo huo unafika mbali kama ilivyokuwa michezo mingine hapa nchini kutokana na kwamba inatoa fursa kwa wanawake kuweza kushiriki kwenye michezo na kupata manufaa.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba mashindano hayo yalianza 2017 yamekuwa yakikumbana na changamoto mbalimbali lakini kubwa ni ukosefu wadhamini na ndio maana kupelekea zawadi kuwa za kususasua.

Hata hivyo alisema pamoja na hayo aliwashukuru wahisani kwa kuendelee kumsapoti na kuwaunga mkono katika mashindano hayo ikiwemo Benki ya NMB, Tanga Women Group, Arbarb Intertainment na Mkulima.

Aliwataja wahisani wengine ni Tanga City Lounge,Dion Pub,Lacosta Pub,Cholloo Spare Party,Quality Class Wear,G1 Security wakatao weza ulinzi,All Stars One 21 huku akiwataka wadhamini kujitokeza kudhamini mchezo huo.

Awali akizungumza Mratibu Mkuu wa Mashindano hayo Zaituni Mango alisema kwamba huo ni msimu wa nne wa mashindano hayo yaliyoanza 2017 .

Alisema msimu huo wa wanne ulianza February 10 mwaka huu na february 13 ndio walianza mashindano kwa timu tisa ambazo ni Magomeni Queen,Costo Ladiers,Mkwakwani Basket,Kwaminchi Queeni,Magomeni Sisiter,Mwarongo,Street Colurs,Tanga Kwanza na Daba, Jangos.

Mratibu huyo alisema kwamba timu hizo zilicheza na baadae kujichuja na kubakia timu mbili ambazo zimeingia kwenye hatua hiyo ya fainali ili kumpata bingwa.

Akielezea suala la zawadi kwa ajili ya washiriki ambapo alisema mshindi wa kwanza ataapata medali za fedha kwa wachezaji saba ,cheti ch ushiriki kwa timu ,Unga wa ngano kg 25,Mafuta ya kupikia lita 10 na fedha taslimu.

Alisema mshindi wa pili medali za fedha kwa wachezaji saba,cheti na ngano kg 15 na mafita lita sita na fedha taslim huku mshindi wa tatu akipata cheti ngano kg 10 mafuta lita 3 na fedha taslimu.


Hata hivyo alisema kwa upande wa mshindi wanne watapata cheti, ngano kg 10 na mafuta lita 3 na fedha na washiriki wote tisa watapata cheti huku mchezaji bora atakapata fedha na mpira utakaotumika kucheza fainali.

Alisema mfungaji bora atapata fedha na kitropiki huku timu yenye nidhamu itapata kikombe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527