ÇHADEMA KUPOTEZA JIJI LA MBEYA BAADA YA MADIWAN WAKE WAWILI KUMTIMKIA CCM | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, March 11, 2020

ÇHADEMA KUPOTEZA JIJI LA MBEYA BAADA YA MADIWAN WAKE WAWILI KUMTIMKIA CCM

  Malunde       Wednesday, March 11, 2020
Madiwani wa CHADEMA Halmashauri ya Jiji la Mbeya Ndg Lucas Mwampiki, Kata ya Mwakibete na Hussein Japhet Wasuha, Kata ya Itagano wametangaza kukihama chama hiko na kujiunga na CCM wakiungana na wenzao 11 waliojiunga awali. 

Kuhama kwa madiwani hao kunafanya idadi ya waliohama kutoka Chadema kwenda CCM kufikia 14 ambapo Januari 26 mwaka huu madiwani 11 wakiongozwa na aliyekuwa mstahiki meya Mchungaji David Mwashilindi walihamia CCM.

Kutokana na kuhama kwa madiwani hao hivi sasa CCM inakuwa na madiwani 17 huku Chadema ikiwa na madiwani 16 hivyo kuifanya Chadema kuipoteza Halmashauri ya Jiji la Mbeya.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post