BURUNDI YAKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KWAMBA HAINA VIFAA VYA KUPIMA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, March 27, 2020

BURUNDI YAKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI KWAMBA HAINA VIFAA VYA KUPIMA CORONA

  Malunde       Friday, March 27, 2020

Burundi imedai watu wanaotumia mtandao wa internet kusema nchi hiyo haina vifaa vvya kugundua virusi vya corona kuwa ni waongo.

Kwenye taarifa iliyotolewa jana jioni, msemaji wa serikali ya Burundi Prosper Ntahorwamiye amesema nchi hiyo ina vifaa vya kutosha na vyenye ufanisi vya kugundua virusi vya corona. 

Ametolea mfano ushahidi kuwa mwalimu kutoka shule inayomilikiwa na Wafaransa aliyeshukiwa kuwa na virusi hivyo amepimwa, lakini matokeo yameonesha kuwa hana virusi.

Serikali ya Burundi imeonya dhidi ya vitendo vya kupotosha ukweli na kutafsiri vibaya maamuzi yaliyotolewa na serikali. 

Msemaji huyo amesema serikali ina madaraka ya kuchukua hatua mwafaka dhidi ya watu wanaotoa kauli zisizo za kweli.

Wakati huohuo, serikali ya Burundi imeshukuru China kwa kutoa vifaa vya kuisaidia kukabiliana na uwezekano wa mlipuko wa virusi vya Corona nchini humo.

Credit: CRI


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post