WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ARIDHISHWA UJENZI WA UZIO WA MAKABURI YA WANANCHI WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA LORI LA MAFUTA MOROGORO


Na Jackline Lolah Minja - Malunde 1 blog
Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameeleza kuridhishwa na ujenzi wa uzio uliowekwa kwenye makaburi ya waathirika wa ajali ya moto uliosabishwa na lori lenye mafuta kuripuka mkoani Morogoro ambao umegharimu shilingi milioni 10 na kuitaka manispaa  ya Morogoro iwe na uangalizi wa sehemu hiyo. 

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne Machi 10,2020 mkoani Morogoro wakati alipotembelea na kukagua eneo hilo ambalo aliagiza lijengwe kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya waathirika wa ajali ya moto. 

"Niliona leo nitumiea siku hii kuja  kukagua na nijiridhishe kwa kazi niliyoagiza zifanyike ambazo ni kazi ya ujenzi wa  uzio ambao niliagiza usiwe wa milioni 33 na badala yake zitumike milioni 10 kwa sababu sikutaka tuchukue nafasi kubwa maana tungepoteza maeneo mengine kwa ajili ya wengine na nimeridhishwa na ukuta pamoja na thamani ya pesa mmefanya vizuri kwa sababu ni ishara nzuri ya kwamba humu ndani kunaonyesha kuna kitu",alisema Majaliwa. 

 Amesema anaunga mkono kuhusu makaburi yote kujengwa kwa mfanano na kujengwa mnara utakaoonyesha ishara ya kuwaenzi waathirika hao wa moto.

Aidha amesema pia kuwepo kwa eneo la wazi ambalo litasaidia kwa wanandugu wanaohitaji kufanya misa au ibada waruhusiwe lakini pia lazima kuwe na kumbukumbu ya mwaka kama ilivyo Kagera. 

"Basi ningeomba kuwa wanandugu wanaotaka kuja kufanya misa waruhusiwe lakini pia kuwe na kumbukumbu ya tarehe hiyo ya tukio ili waje mwenye kuweka mashada maua na kutoa dua kwa imani yake na eneo hilo lilindwe," alisisitiza Majaliwa. 

Hata hivyo amesema kuwa ametoa kibali cha kuendelea kwa ujenzi na kusisitiza kuwa yanapotolewa maagizo yakitekelezwa kama hivyo inapendeza.

Waziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  akizungumza baada ya akieeleza kuridhishwa na ujenzi wa uzio uliowekwa kwenye makaburi ya waathirika wa ajali ya moto uliosabishwa na lori lenye mafuta kuripuka mkoani Morogoro.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post