BIBI WA MIAKA 80 ABAKWA HADI KUFA, AKATWA VIUNGO

Picha haihusiani na habari hapa chini
Kikongwe anayekadiriwa kuwa na zaidi ya miaka 80, mkazi wa Kijiji cha Shaurimoyo wilayani Babati, amebainika kubakwa na kuuawa na hatimaye kukatwa vidole na watu waliomfanyia unyama huo.

Kikongwe huyo alikutwa amekufa Machi 8, 2020 baada ya kufanyiwa ukatili na watu wasiojulikana.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kikongwe huyo alikutwa amekatwa vidole na kitu chenye ncha kali na kubakwa hali ambayo inaelezewa kuwa huenda ilisababisha kupoteza maisha. 

Bibi huyo (jina linahifadhiwa) pia alikutwa akiwa amekatwa sehemu ya unyayo jambo ambalo limehusishwa na imani za kishirikina.

Majirani wa bibi huyo aliyekuwa akiishi peke yake, walisema mwili wake pia ulikutwa ukiwa umekatwa sikio na vidole vya mkono. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Shaurimoyo, Dismas Dodo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wanakijiji, alichukua hatua ya haraka ya kuwasiliana na Jeshi la Polisi Kituo Kdogo cha Magugu.

Diwani wa Kisangaji, Adamu Ipingika, akiwa kwenye msiba wa kikongwe huyo juzi, alikemea kitendo hicho na kuwataka wanakijiji kutoa ushirikiano kwa polisi ili watuhumiwa waliofanya uhalifu huo wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisangaji, John Jacob, alisema katika mwezi huu, mtoto wa miaka minne alibakwa katika kijiji hicho na mtuhumiwa mwenye miaka 30 lakini alikamatwa na kufikishwa katika Kituo Kidogo cha Polisi Magugu.

Soma zaidi <<HAPA>>

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post