ATCL YAFUTA SAFARI KWENDA COMORO, UGANDA, BURUNDI KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, March 24, 2020

ATCL YAFUTA SAFARI KWENDA COMORO, UGANDA, BURUNDI KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA

  Malunde       Tuesday, March 24, 2020
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imefuta safari zake za kwenda nchini Comoro, na hivyo kuifanya iwe imefuta safari zake kwenda kwenye mataifa manne tangu kutokea kwa mlipuko wa virusi vya corona katika mataifa mbalimbali duniani.


Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kuwa ndege ya ATCL inafanya safari yake ya mwisho hii leo kutoka Dar es salaam kwenda Comoro, na baada ya hapo abiria ambao tayari wamekata tiketi kwa ajili ya safari watarudishiwa fedha zao bila chaji yoyote ya ziada.

Safari nyingine zilizofutwa na ATCL kwenda nje ya nchi ni pamoja na ile ya kwenda Mumbai nchini India baada ya serikali ya nchi hiyo kuzuia wageni kuingia nchini humo hadi Aprili 15 mwaka huu, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Safari nyingine zilizofutwa na ATCL ni ile ya kutoka Dar es salaam kwenda Entebbe Uganda na ile ya kutoka Dar es salaam kwenda Bujumbura Burundi, sababu ikiwa ni hiyo hiyo ya mlipuko wa virusi vya corona.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post