AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA BAADA YA KUMBAKA NA KISHA KUMNYONGA BINTI WA MIAKA 7


Mtuhumiwa  anayedaiwa kubaka mtoto wa umri wa miaka 7, kisha kumnyonga shingo hadi kumuua amehukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma kunyongwa hadi kufa.

Aliyehukumiwa kifo, ni Matiko Chanduru (20) mkazi wa Kijiji cha Maburi wilayani Serengeti mkoani Mara,aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia namba 27/2019 ambayo iliharishwa kutolewa hukumu kutokana na utata wa umri ambao sasa umethibitishwa na daktari kwamba ni mtu mzima.

Kabla ya kutolewa hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma, John Kayohoza alimkumbusha mshtakiwa shtaka lililokuwa linamkabili la kubaka kwamba alitenda kosa hilo Juni 30, 2018 nyakati za jioni Kijiji cha Maburi eneo la Mlima Ujerumani,akilinda shamba kuzuia wanyama waharibifu kwa kumbaka Munira Frahimu(7).

Binti huyo,ambaye anamuita mshtakiwa mjomba, alimbaka na kumsababishia maumi vu makali sehemu za siri baada ya kufanyiwa ukatili huo,alijikokota kwenda kwa bibi yake anapoishi na kumweleza mjomba mkubwa Asante Chanduru kuhusu kitendo alichofanyiwa.

Mjomba wake, aliamua kwenda kumhoji akiwa na binti huyo, lakini mtuhumiwa alikataa

Baada ya muda inadaiwa mtoto  aliondoka kurejea nyumbani ,akiwa njiani kurudi kwa bibi yake, mshtakiwa alimfuatilia kwa nyuma na kumkamata kwa nguvu,kisha kumvutia vichakani na kumnyonga shingo na kumvua nguo zote na kubakisha nguo ya ndani ambayo aliiteremsha hadi kwenye ma goti na kutupa mwili porini.

Ilielezwa Julai mosi,2018, mtuhumiwa baada ya kubanwa na uongozi wa kijiji pamoja na ndugu, alikiri kutenda kitendo hicho na kuwapeleka hadi alipotelekeza mwili  wa mpwa wake, kisha kufikishwa mahakamani.

Mahakama baada ya kumkumbusha mshtakiwa kosa na kuthibitisha, alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na si vinginevyo na kusema mtuhumiwa anaweza kukata rufaa ndani ya siku 30 kama hakuridhika na hukumu hiyo.

Credit: Mtanzania


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post