43 WAFARIKI KWA VIRUSI VYA CORONA IRAN....WANANCHI WATAKIWA KUSALIA MAJUMBANI | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, March 1, 2020

43 WAFARIKI KWA VIRUSI VYA CORONA IRAN....WANANCHI WATAKIWA KUSALIA MAJUMBANI

  Malunde       Sunday, March 1, 2020

Idadi ya waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Iran imefikia watu 43 na kuwa taifa la pili lenye idadi kubwa ya vifo nje ya China. 


Msemaji wa wizara ya Afya ya Iran amearifu kuwa watu 9 wamekufa kutokana na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita na visa maambukizi vimepanda na kufikia watu 593. 

Serikali mjini Tehran imeamuru kufungwa kwa shule zote hadi siku ya Jumanne na kurefusha likizo ya vyuo vikuu pamoja na kupiga marufuku matamasha na shughuli za michezo kwa wiki moja. 

Maafisa kadhaa wa ngazi ya juu akiwamo makamu wa rais, naibu waziri wa afya na wabunge 5 wamethibitika kuambukizwa virusi hivyo na kuilazimisha serikali kulifunga bunge pamoja na kuweka marufuku ya kusafiri.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post