WAWILI KORTINI KWA KUJILAWITI NA KUSAMBAZA PICHA ZA NGONO

Watu wawili jana February 17, 2020 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kulawiti na kusambaza picha za ngono mtandaoni.


Washatakiwa hao wakazi wa Dar es salaam ni Aisha Juma (Video Vixen) na Mfanyabiashara Samwel Philemon 

 Aisha anadaiwa kusambaza video za ngono Desemba 12,2019 katika maeneo tofauti Dar na Samwel katika siku isiyojulikana na mahali pasipo julikana anadaiwa kumuingilia Aisha kinyume na maumbile huku akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Hakimu Chaungu ametoa masharti ya dhamana ya Tsh. Million 10 ambapo washtakiwa hao wameshindwa kutimizia, kesi imeahirishwa hadi February 26,2020 na washtakiwa wote wamerudishwa mahabusu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527